Pole pole pole pole Pole pole moyo wangu Masikini pole Pole mtima wangu
Haikuwa dhamira Haikuwa kusudi langu Haikuwa dhumuni waala Haikuwa malengo yangu Ila tuseme labda moyo Pengine sio ridhiki Maana nimejitahidi sana Malengo hayafiki
Kama kuswali naswali sana Mpaka sunna za usiku Kazi nimetafuta saana Ila siambulii kitu Sitaki kukufuru mungu Sababu najua ni mapito Japo inakatisha tamaa Ila siku yangu ipoo moyo
Usiumiee (moyo wangu) Ni mapito (ooh moyo) Haya yote mitihani na yana mwisho Moyo wangu moyo Usiumie (moyo) Ni mapito (ooh moyo) Haya yote mitihani na yana mwisho
Penzi maua Pesa mbolea Hata shemeji yako Ana Mengi ila hawezi ongea
Moyo Najitahidi jiepusha vya watu ni majaribu aah Japo nna shida ila naepuka tamaa Moyo nlitamani siku moja na mimi nimjengee mama Ila ndo vile tu umasikini, mipango inakwama Hua naumia watoto shuleni wakifukuzwa ada Najiona mjinga yani sio bora baba Sitaki kukufuru mungu, najua ni mapito Maana riziki mafungu, nami langu siku lipo Moyo
Usiumie (moyo wangu) Ni mapito (ooh moyo) Haya yote mitihani na yana mwisho (Moyo wangu moyo) Usiumie (jikaze moyoo) Ni mapito (ooh moyo) Haya yote mitihani na yana mwisho Moyo ooh Moyo ooh, ooh