Hum, eti nikuombee mema
Na baraka uzidi fanikiwa
Siwezi kamwe wala
Hum, ni sawa na kuiforce sinema
Kuitazama na haijanivutia
Lazima tu ntalala
Ooh, na kwa barabara ukipita
Nenda kulia ukiniona kushoto
Sitaki hata tuonane
Hum, usije wala ukaniita
Donda vilia utanchochea tu moto
Nisije nkutukane, hum
Kinachoniumiza nafsi
Kunisikitisha kwa watu kujishongondoa
Kumbe mapenzi hisabati wakati nayazidisha
Mwenzangu nje unayatoa
Wewe cement mimi mchanga
Nkasema penzi tujenge lisije loa
Najitia mkandarasi naezeka mabati
Wewe chini kenchi unabomoa
Niache
Niache
Niaache (ooh niache)
Niache (niia)
Niache (mimi moyo wangu una hasira)
Niaache (oh niache)
Niache (ooh, oh, oh)
Najitahidi nisilale kwenye kitanda
Huenda ntapunguza ndoto zako, hum
Mwilini nina machale utadhani mwanga
Yote kuusahau uwepo wako, hum
Laiti kama ningekuwa gari
Ningekugonga barabarani
Ama nyuki mtoa asali
Nkung'ate sura wasiitamani
Hivi wewe ungo ulivunja mwali
Ama ulivunja sahani
Kuniundia mateam kwa mitandao
Vijembe vya kazi gani
Kinachoniumiza nafsi
Kunisikitisha kwa watu kujishongondoa
Kumbe mapenzi Hisabati wakati nayazidisha
Mwenzangu nje unayatoa
Wewe cement mimi mchanga
Nkasema penzi tujenge lisije loa
Najitia mkandarasi naezeka mabati
Wewe chini kenchi unabomoa
Niache (ooh niachee)
Niache (mimi moyo wangu una hasira)
Niaache (tena ukae mbali)
Niache (ooh niachee)
Niache (usiwapigie rafiki zangu)
Niache (usithubutu hata simu yangu)
Niaache (chonde tafadhali)
Niache (niiaa)
(Iyoo Lizer)
Hum
Ntakudanganya kwa tabasamu
Ntakudangany kwa kucheka
Ntakudanganya hata kwa salamu
Ila moyoni nakuchukia
Nitakudanganya kukufollow
Nitakudanganya kucomment
Nitakudangaya kulike picha
Ila siwezi kukuzimia