Natoka zangu kwetu kibiti Naisaka dar es salaam Naenda tafuta riziki Niwatunze baba na mama Nikizunga haba na haba Ndio kilo inatosha Chunga miguu kuvaa rubber bana Zisizo kutosha Anayesema riziki mafungu saba Anakupotosha Riziki mafungu mawili Kupata au kukosa Aliyoyasema baba Heshima ya nyumba si dirisha Dunia ni saa mbovu mwana Usije ifwatisha Vingine vinakaba Lazima unywe maji kupitisha Umia upate kovu baba Maumivu yatakwisha
Hata mate kinywani ya uchungu Nayameza kwa tabu jama Maisha yangu mazingaombwe Ya maajabu sana Oooh mama oooh Eeeeh mama eeeh
Najipa matumaini Nitafute nisichoke Moyoni nikiamini kuwa Mungu ni wetu sote Ila mbona kwangu sasambu sasambu Sipati usiku si mchana Ama kitabu cha riziki yangu Tayari kimechanwa Eeeeh eh eeeeh Baba mama chama na mogela Yani mimi ndio nategemewa Nakaza nashinda kombolela Likipigwa nabutua hewa
Hata mate kinywani ya uchungu Nayameza kwa tabu jama Maisha yangu mazingaombwe Ya maajabu sana Oooh mama oooh (oooh) Eeeeh mama eeeh (oh oooh)