Usidate na njonjo za mapenzi Vicheko bandia usoni kudeka kumbe Ana pretend Maufundi toka Tanga na Zenji Vionjo mitego unase ashike pochi umwage chenji
Anakuchanganya kiunoni shanga Marashi kama uko peponi Mtoto sauti kinanda Ya kumtoa chatu pangoni Ukishatafuna karanga Hutaki hata aende sokoni Anakuchuna mafaranga Unabaki na vumbi mfukoni
Ukiwa na pesa utasifiwa kitambi Baby me I like that Nakukupamba kwenye simu Video Snapchat Kumbe hana maana hadi mangi Anamwita sweetheart Kisa anakesha gym Kutafuta six packs
Unaibiwa Unaibiwa Unaibiwa Unaibiwa
Kuna kina Rose Visosa Wale wapenda Verosa Ukipita na shati na moka Lazima watashoboka Wakiomba lift, ogopa Miguu dashboard vishoka Mchunguze cheni, goroka Nywele na pochi kakopa, eh
Usije kuyavamia yasije yakakutesa Hawachelewagi kukimbia Kuna wenzako wanalia Walizani mapenzi pesa Kwenye suruali vibamia
Hata ukimuonga Ferrari Hatokuona rijali Wakati chumbani we beki Ukifunga moja tu chali Atakamatwa na mangangali vijana machachali Hawachagui sehemu ya vita uvunguni na juu ya dali
Ukiwa na pesa utasifiwa kitambi Baby me I like that Nakukupamba kwenye simu Video Snapchat Kumbe hana maana hadi mangi Anamwita sweetheart Kisa anakesha gym Kutafuta six packs
Unaibiwa Unaibiwa Unaibiwa Unaibiwa
Unadhani niwapekeako Kumbe wengine wameshaweka kambi Kakupendea macho Wapo wengine kawapendea rangi Ye ni gari la dampo Hachagui taka dereva mpe ganji Wakubadili sample Akila mihogo karoti hazipandi