Yani kwa sauti Kasema deeka deeka Na mimi najiachia Kanipa shuruti La kumteka teka Silaha kanigawia Mbezi kimara Hunipeleka peleka Mpaka mwisho hashuki hashuki Kiungo imara Hunipenyeka penyeka Kwa ya nguvu mashuti mashuti
Ooh oh! Kaniweka darasani Kunifundisha vizuri Mengi hayajulikani Yataka kuyakariri Kanichorea ramani Kopa lenye nyingi siri Jekundu nje na ndani Rangi yake zingifuri
Raha kupendwa raha Mhh! Kupendwa raha Raha jamani raha Naona raha Raha (raha) Kupendwa raha Ooh! Kupendwa raha Raha jamani raha
Eti niende msituni Zaraninge na matipwili nikamroge Abadan (abadaan) Penzi nichanjie mizaituni Kwa vilinge na kuzikiri Linoge Aah abadan aah abadan Mmhh! Vineno vya kisirani Kafumwa na mwafulani Mweupe mara kijani Inawahusu nini? Vipimo viso mizani Kutwa kwenu midomoni Tumewakaa kichwani Mtumezee kwinini
Ndege asili ya buga Kufugwa hawezekani Mithili ya kivuruga Kaumbiwa kutamani Atenda tafuta boga Japo tama libandani Ende tezi sina woga Atarejea ngamani
Raha kupendwa raha Mmhh! Kupendwa raha Raha jamani raha Naona raha Raha (raha) Kupendwa raha Ooh! Kupendwa raha Raha jamani raha